Karibuni - Welcome!
Karibuni kwa tovuti rasmi ya Chama cha Michezo ya Jadi - Mkoa wa Dar es Salaam.

 

Lengo kuu la tovuti hii ni kuwawezesha watu wote duniani kupata habari kuhusu michezo ya jadi ya Tanzania, hasa mchezo wa bao.

 

Tunakuomba sana uutupatie maoni na mapendekezo yako.

 
Historia fupi ya Chama cha Michezo ya Jadi - Mkoa wa Dar es Salaam

Baada ya kupata Uhuru Chama cha TANU kwa kupitia Serikali ya awamu ya kwanza ikiweka azimio la kufufua michezo ya jadi. Kukaundwa Chama cha Michezo ya Jadi cha Taifa (CHAMIJATA) mwaka 1976.
Mashindano ya kwanza ya Taifa yalifanyika Dodoma mwaka 1975.
Michezo iliyoshindiwa ilikuwa mieleka, kutupa mikuki, kulenga kwa mishale na bao.

bao kubwa Chama cha Michezo ya Jadi Mkoa wa Dar es Salaam (CHAMIJADA), kilichoanzishwa na Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Baba wa Taifa Hayati Mwl J.K Nyerere, kimedhamiria kuufufua, kuukuza na kuuendeleza Michezo wa Bao kufikia hatua ya kuwa Mchezo wa Kitaifa na alama ya Taifa letu hatimaye kuwa moja ya Michezo ya Kimataifa.
CHAMIJADA ni chama kinachosimamia na kuratibu shughuli zote za michezo ya jadi mkoani Dar es Salaam, ni chama halali ambacho kinaendesha shughuli zake kisheria, kimesajailiwa kwa mujibu wa sheria ya Baraza la Michezo la Taifa (NSC) kifungu namba 12 ya mwaka 1967 na marekebisho yake na 6 ya mwaka 1971.
Katika jitihada hizi Chamijada imetunga sheria za mchezo na kuzifanyia marekebisho mbalimbali katika mashindano yaliyoandaliwa yakiwemo Mashindano ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere.
Chamijada imezifanyia utafiti kwa miaka minne mfululizo na kuzipeleka kwa wadau katika manispaa Temeke, Ilala na Kinondoni kwa kuzijadili na kutoa maoni yao hatimaye kuzipitisha.
Kwasa sheria hii zinakidhi haja ya kuendesha na kuuongoza Mchezo na kutoa maamuzi bila kuleta athari upande wowote.
Baraza la Michezo la Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake ambaye ni Katibu tawala wa Mkoa Ras lilimteua Ndg Monday Likwepa kuwa Mwenyekiti mtendaji wa Chamijada tangu 2003 na amepewa majukumu matano (5) ya kufanya na kamati yake nzima kabla ya kuitisha uchaguzi.

 

shindano Shindano la Bao
Torino (Italia)
22-23/11/2008